Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) Tanzania, ametembelea walimu na wanafunzi nchini Burundi katika ziara ya kikazi na kiroho. Katika ziara hiyo, alifanya mazungumzo na walimu pamoja na wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali ya kielimu, hususan programu za masomo na malezi ya kiroho. Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa kielimu na kuboresha mifumo ya ufundishaji na malezi katika taasisi hiyo iliyopo chini ya Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) ndani ya nchi hiyo (ya Burundi) inayopakana na Rwanda upande wa Kaskazini, na Tanzania upande wa Mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo upande wa Magharibi.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) Tanzania, amepata Tawfiq ya kufanya muhimu ya kitaaluma na kiroho Nchini Burundi. Ziara hii ilifanyika katika mazingira ya upendo, maadili na hali ya kiroho ya hali ya juu.
Katika ziara hiyo, Dkt. Taqavi alikutana na kufanya mazungumzo na walimu pamoja na wanafunzi, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kielimu na masomo yanayotolewa.
Aidha, walipitia na kujadili programu tofauti za chuo, hususan programu za malezi ya kiroho na maadili.
Ziara hii imelenga kuimarisha uhusiano wa kielimu na kiroho kati ya viongozi na wanafunzi, pamoja na kuboresha ubora wa programu za ufundishaji na Malezi Matukufu ya Kiislamu.
Your Comment